Naibu Waziri Gekul awataka wasanii kutumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi zao badala ya mambo binafsi

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amewataka Wasanii nchini kuitumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kutangaza kazi zao ili zifahamike, kukuza sekta ya Sanaa nchini na kuwaletea maendeleo badala ya kutangaza mambo yao binafsi ambayo hayana tija,anaripoti Grace Semfuko (MAELEZO).

Pia amewataka Wazazi wa Wasanii kulinda hadhi za watoto wao kwa kutowahusisha kwenye migogoro yao ya mahusiano pindi baba na mama wanaporafakakana kwani wanawaingiza kwenye historia isiyofaa katika maadili ya Kitanzania.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul, akizungumza na Watendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), alipotembelea ofisi hizo zilizoko Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kupata taarifa za utendaji wa Taasisi hiyo, Mhe. Gekul ameanza ziara ya kutembelea taasisi za Wizara ya Habari tangu aapishwe kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Aprili 1, 2021.

Mhe. Gekul ameyasema hayo katika ziara yake kwenye Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kulitaka Baraza hilo kuongeza umakini katika kusimamia na kuimarisha maadili na mienendo ya wasanii nchini.

Kama kuna kitu Watanzania hawaridhishwi nacho ni kitendo cha msanii kuelezea maisha yake binafsibtena katika mambo ambayo hayana tija. Umakuta Msanii anaweka taarifa zake binafsi mitandaoni kwamba nimezaa na huyu, nina wanawake kadhaa…hii inadidimiza utamaduni wetu, wanatuharibia kizazi hiki ambacho kinakua kuona kwamba ni fasheni kueleza mahusiano kwenye mitandao, ameeleza Gekul. Aidha amesema ni muhimu Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Sanaa zikasimamiwa ipasavyo ili kuhakikisha wanaondokana na vitendo hivyo ambavyo amevitaja kuwa vinashusha hadhi ya Wasanii nchini.

Hivi hakuna Sheria inayowabana, si ipo? au adhabu na fine zimekuwa ndogo sana? Tunasimamia kwa kiasi gani hizo kanuni?, amehoji Mhe. Naibu Waziri na kueleza kuwa watanzania wanatamanikuwafahamu Wasanii wao kwa mambo mazuri ya kujenga jamii zetu na si kwa mambo yao binafsi.

Kuhusu Wazazi wa Wasanii kuingiza Vijana wao kwenye migogoro ya mahusiano ya kifamilia, Gekul amesema ni muhimu mzazi kulinda hadhi na maslahi ya mtoto wake kwa kumuondolea historia isiyofaa kwa jamii inayomzunguka na kwamba ni muhimu kuzingatia maadili ya kitanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news