Rais Samia afanya uteuzi leo Aprili 17, 2021 miongoni mwa wateule ni Mndolwa kuwa Balozi, Ndomba kuwa Mkurugenzi eGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amemteua Yusuf Tindi Mndolwa kuwa Balozi na pia kuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.


Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Operesheni wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Benedict Benny Ndomba kuwa Mkurugenzi wa  Mamlaka hiyo (eGA).


Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dodoma usiku huu, imesema, Balozi Mteule Mndolwa anachukua nafasi iliyoachwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


"Balozi Mteule Mndolwa ataapishwa Jumatatu  Aprili 19, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma,"imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa Ndomba ambaye uteuzi wake umeanza  leo Aprili 17, 2021, anachukua nafasi ya nafasi ya Dk. Jabir Bakari Kuwe ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 17 Aprili, 2021.


Post a Comment

0 Comments