Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo Aprili 19, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;

1.   Amemteua Dkt. Richard J. MASIKA kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili, 2021.  Dkt. MASIKA anachukua nafasi ya Marehemu Prof. Apollinary Elikana PELEKA.

 

2.   Amemteua Prof.  Joseph J. MSAMBICHAKA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).  Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.  Prof. MSAMBICHAKA anachukua nafasi ya Prof. Manase Peter SALEMA.

 

3.    Amemteua Dkt. Revocatus Petro MUSHUMBUSI kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).  Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili, 2021.  Dkt. MSHUMBUSI anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladislaus NSHUBEMUKI ambaye amestaafu.

 

4.   Amemteua Prof. John W.A. KONDORO kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.

 

5.   Amemteua Dkt. Mboni A. RUZEGEA kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili, 2021.  Dkt. RUZEGEA anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ali MCHARAZO ambaye amestaafu.

 

6.   Amemteua Prof. Esther Hellen LUGWISHA kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.

 

7.   Amemteua Kept. Ernest Mihayo BUPAMBA kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (Dar es Salaam Maritime Institute – DMI) baada ya kumaliza kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.

 

8.   Amememteua Prof. Makenya MABOKO kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.
Post a Comment

0 Comments