RAIS SAMIA AMEKATA KIU

Napenda niungane na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya 5, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa hotuba safi iliyokata kiu na matarajio ya Watanzania,anaandika Emmanuel J. Shilatu.
Rais Samia ametumia dakika 90 kutoa mwelekeo mzuri wa Serikali yake kwa kuchambua vyema tulipotoka, tulipo na tunapokwenda kwa kuonyesha nia ya dhati ya kazi iendelee kweli kweli kivitendo kwenye sekta zote muhimu zinazogusa maslahi na maisha ya Watanzania.

Rais Samia amepigilia vyema msumari wa mwendelezo wa kazi, maono ya Hayati Dkt Magufuli kwa kuendeleza miradi ya kimkakati; mapambano ya dhati dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na ubadhirifu wa mali za umma. Hakika Rais Samia na Hayati Dkt. Magufuli walikuwa kitu kimoja, mwendo ni ule ule.

Suala zima la kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, kuondoa urasimu, kuokoa mashirika na kujisahihisha ili kwenda mbele kwa mafanikio makubwa kwa mwendo zaidi ya ule wa awali.

Narudia tena kumpongeza Rais Samia kwa kukata kiu ya Watanzania, kazi iendelee.

Post a Comment

0 Comments