Rais Samia ateua viongozi mbalimbali leo usiku wa Aprili 22, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 22, 2021 amefanya teuzi mbalimbali kama ifuatavyo;

Rais Samia Suluhu amemteua  Prof. Henry Mahoo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, amemteua pia Prof. Aurelia Kamuzora kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania.

Rais Samia amemteua pia Jaji wa Mahakama ya Rufani Dkt. Gerlad Ndika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Rais Samia amemteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania, Kikula ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya cha kwanza kumalizika, Rais amewateua pia Prof. Abdulkarim Mruma na Janeth Lekashingo kuwa Wajumbe wa Tume ya Madini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments