Rais Samia ateua viongozi wawili leo Aprili 23, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 23, 2021 amefanya uteuzi kama ifuatavyo;

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, leo, imesema, Rais amemteua pia Sophia Elias Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Jira katika Utumishi wa Umma (PSRS).

Taarifa imefafanua kuwa Dkt. Swai ameteuliwa kushika wadhifa wa kuwa Mwenyekiti wa TACAIDS kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

"Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2021,"imeeleza taarifa hiyo.Post a Comment

0 Comments