Rais Samia atunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi 386 wa jeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 17, 2021 amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 386 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 17 Aprili, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Zoezi hilo limefanyika leo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ikiwa ambapo kundi la kwanza la mwaka 2017 lilitunukiwa shahada ya sayansi ya kijeshi  na kundi la pili namba 68 walitunukiwa kozi ya mwaka mmoja.

Sehemu ya Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 kabla ya kutunukiwa Kamisheni katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 17 Aprili, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 17 Aprili, 2021.

Aidha, ni mara kwa kwanza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutunuku kamisheni tangu aapishwe kushika wadhifa huo Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 17 Aprili, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 17 Aprili, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 leo tarehe 17 Aprili, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika uwanja wa Gwaride kwa ajili ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 leo tarehe 17 Aprili, 2021 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Generali Jackson Jairos Mwaseba haonekani pichani mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kutunukua Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 leo tarehe 17 Aprili, 2021. (Picha zote na Ikulu).

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kundi la kwanza lina askari 158 na wote ni Watanzania na kati yao wanaume ni 150 na wanawake wanane.

Pia amesema waliokatisha mafunzo ni 15 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, kushindwa kufikia viwango vya ufaulu, kukimbia mafunzo na utovu wa nidhamu.

Mkuu huyo amesema kundi la pili lilikuwa na maofisa 244 na kati yao 237 ni Watanzania huku nchi rafiki ikiwemo Eswatini maofisa watano, Kenya maofisa wawili jumla wanakuwa 244.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 17 April 2021 amehudhuria Hafla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa JWTZ na Mahafali ya kwanza ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa Maafisa Wanafunzi kundi 01/17 Ikulu Chamwino Dodoma.

Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma

Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 wakila Kiapo cha Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

 Maafisa Wanafunzi 143 kundi la 01/17 ambao wametunukiwa Kamisheni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakiondoka katika viwanja vya Ikulu huku wakiwa wametengeneza umbo la Omega kuashiria mwisho wa Mafunzo yao leo tarehe 17 Aprili 2021.

Post a Comment

0 Comments