Serikali yataja inavyopima utendaji wa wakurugenzi katika halmashauri

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao.

Akikagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga Waziri Ummy amesema kila Halmashauri ina wajibu wa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Amesema Halmashauri inatakiwa kutenga fedha za maendeleo kutoka katoka mapato yap ya ndani ili kutatua changamoto za wananchi katika sekta ya afya, elimu na Ujenzi wa miundombinu na miradi mingine.

Anaendelea kusema kuwa Halmashauri kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ni jambo moja lakini kutelekeza miradi hiyo ni jambo lingine na Wakurugenzi wanapaswa kusimamia ipasavyo ili miradi hiyo iweze kuleta mabadiliko katika jamii.

Wakati huohuo Waziri Ummy amewaagiza Wahandisi wa Mikoa, Halmashauri na TARURA kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia na kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Halmashauri zao ili kuhakiki ubora wa majengo hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news