Serikali yawataka waliohamisha fedha benki kuzirejesha

Serikali imetoa rai kwa wafanyabiashara wote waliotoa fedha zao kwenye mabenki wakiogopa zitachukuliwa baada ya akaunti zao kuonekana na fedha nyingi kuzirejesha kwa hiari na kuendelea na utaratibu wa kutumia benki kutunza fedha zao.

Pia imewataka watendaji walio na jukumu la kukusanya kodi kuhakikisha wanakusanya kodi kwa wafanyabiasha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwa kuchukua kiasi cha kodi kinachohitajika kisheria na si kuuwa shughuli ama biashara kwa kuchukua fedha zisizostahili.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha kuchakata maelekezo yaliyotolewa kwa wizara hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akipokea taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) na wakati wa hotuba iliyoitoa wakati kuwaapisha viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na manaibu.

Mwigulu amesema jukumu la serikali suala la ukusanyaji wa kodi linaonekana haliko sawa na limekuwa mjadala mkubwa hata bungeni, alisema ukitaka kukusanya kodi kwanza lazima wakuze uchumina kuulinda ili kuapata wigo mpana wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara nchini.

Kuhusu umuhimu wa ulipaji wa kodi kwa mlipa kodi, ametoa onyo kwa walipa kodi ambao wamekuwa na janja janja ya kulipa kodi kuacha tabia hiyo mara moja, maana kukwepa kodi ni kuvunja sheria na ni jambo ambalo halivumiliki kwa kwa serikali. (Matokeochanya).

Post a Comment

0 Comments