Simba SC yainyemelea Yanga SC kileleni yatembeza 2-0 kwa Kagera Sugar

Wekundu wa Msimbazi Simba SC watwaa alama tatu katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliowakutanisha na Kagera Sugar leo Aprili 21, 2021, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Kagera).

Ushindi huo umesindikizwa na mabao mawili kwa bilakatika dimba la Kaitaba mkoani Kagera ikiwa ni mwendelezo wa mitanange ya mabingwa huo katika Ukanda wa Ziwa.

Luis Miquissone  ndiye alieanza kuandika bao timu yao hiyo ndani ya dakika 12 baada ya kupokea  pasi nzuri kutoka kwa Clatous Chama.

Aidha, Chriss Mugalu alitonesha kidonda cha Kagera Sugar ndani ya dakika 23 baada ya kupachika bao la pili kutokana na kazi nzuri aliyopewa na Hassan Dilunga ndani ya dimba hilo.

Katika mtanage huo Kagera Sugar waliwatoa Abdallah Mfuko, Peter Mwalyanzi na Mwaita Gereza huku Dickson Mhilu, Saadat Nanguo,  na Hassan Mwatarema wakiingia ili kuongeza nguvu.

Post a Comment

0 Comments