TAKUKURU Arusha yawafikisha mahakamani watumishi sita kwa rushwa, uhujumu uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha imewafikisha mahakamani watumishi sita kwa makosa ya rushwa na uhujumu wa uchumi kwa kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Karatu hasara ya zaidi ya sh.milioni 11,anaripoti Pamela Mollel.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Arusha, James Ruge amesema kuwa ofisi ya Takukuru kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka imefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Tarafa ya Eyasi wilayani Karatu.

Amesema kuwa, washtakiwa hao wanatuhumiwa kuisababisha hasara hiyo kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018 ambapo walihusika kukussnya kiasi cha zaidi ya sh.milioni 11 lakini hawakuwasilisha katika mamlaka husika.

Wakati huo huo taasisi hiyo imewafikisha mahakamani watuhumiwa wengine watatu wakazi wa Longido kwa kosa la kutumia nyaraka za uongo.

Aidha Ruge ameongeza kuwa katika tukio lingine taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya sh. milioni kumi zikizokuwa zimechepushwa na kufanyiwa ubadhirifu kinyume na sheria ,fedha ambazo zilikuwa stahiki za waliokuwa watumishi wa World Vision mkoani Arusha.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, James Ruge (kushoto) akikabidhi fedha zilizokuwa zimechepushwa na kufanyiwa ubadhilifu kinyume na sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007, fedha ambazo zilikuwa ni stahiki za waliokuwa wafanyakazi wa Word Vision mkoa wa Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

Previous Post Next Post

International news