TSC YAHAMASISHWA KUHAKIKISHA WALIMU HAWAONDOKI KAZINI

Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wamehamasishwa kubuni mbinu zitakazowafanya walimu waache kukiuka maadili ya kazi yao, suala ambalo husababisha wengi kupata adhabu mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kazi, anaripoti Veronica Simba (TSC) Mwanza.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi, akifungua mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza. Kulia ni Mwenyekiti wa TSC Prof. Willy Komba.

Wito huo umetolewa Aprili 28 mwaka huu na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi, wakati akifungua mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.

“TSC hakipaswi kuwa chombo cha kusubiri mashauri. Lazima muwe na utaratibu wa kuhakikisha walimu hawafanyi makosa yanayosababisha kuondolewa kazini,” alisisitiza.

Kuhusu suala la maadili, Mwl. Nkwabi ameishauri TSC kuzifikia shule zote kwa lengo la kuhakikisha walimu wanazingatia maadili ya kazi yao kwa kuwalea vema wanafunzi ili wawe raia wema.

Alisema kuwa ni wajibu wa walimu kusimamia maadili na makuzi ya wanafunzi hivyo TSC ikiwa ni Mamlaka yao ya Nidhamu, inapaswa kuhakikisha wajibu huo unatekelezwa kikamilifu.
Mshiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.

Afisa Elimu huyo alikemea tabia ya baadhi ya walimu kuwachukulia wanafunzi kama wateja wao hivyo hawashughuliki na malezi yao wakiamini kuwa mteja hakemewi kwani ndiye anawawezesha kupata mshahara.

“Siku walimu wote wakiwaangalia wanafunzi kama watoto wao wa kuzaa, tunaweza kuondokana na tatizo hili.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TSC Prof. Willy Komba, akitoa neno la kumkaribisha Mgeni Rasmi, aliwaasa watendaji wa Tume hiyo kuhakikisha wanatenda haki kwa walimu kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo, ili nao waweze kuwalea wanafunzi vema.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Prof. Willy Komba, akitoa neno la kumkaribisha Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi, ili afungue mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.

“Walimu bora ndiyo watazaa elimu bora. Walimu bora lazima wahudumiwe vizuri. Bila kuwahudumia walimu vizuri watakuwa na manung’uniko na kero na hawatafanya kazi vizuri. Ndiyo maana Serikali ikatuamini sisi tuwahudumie,” alisisitiza Prof. Komba.

Akitoa neno la utangulizi, Katibu wa TSC, Mwl. Paulina Nkwama alitoa shukrani kwa Mungu na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kushika wadhifa huo, hivyo aliahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu na weledi ili asimwangushe Rais.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Mwl. Paulina Nkwama, akitoa taarifa ya utangulizi kabla ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi, kufungua mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.

Akizungumzia mafunzo husika, Mwl. Nkwama alieleza kuwa ni zoezi endelevu ambalo litaendelea katika Kanda zote saba zinazohudumiwa na TSC kwa lengo la kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati husika waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.

“Ni matarajio yetu kuwa baada ya mafunzo haya, Wajumbe wa Kamati husika wataenda kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu, ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao ya kuwalea wanafunzi ipasavyo kimwili na kiroho.
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Suzan Nussu akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameshirikisha Wajumbe kutoka Wilaya zote za Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambazo ni Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama, akiwasilisha mada kuhusu Muundo na Majukumu ya Tume hiyo wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Christina Hape, akiwasilisha mada kuhusu Kusudi la kuanzishwa kwa Tume hiyo wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.
Mshiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.
Mshiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.
Mshiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.
Mshiriki wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zilizoko Kanda ya Ziwa akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza, Aprili 28, 2021.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Shani Kamala akizungumza jambo wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mectildis Kapinga, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume kuhusu masuala ya ajira na maendeleo ya walimu wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Richard Odongo, akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa Kamati za Wilaya za TSC zilizoko Kanda ya Ziwa, Aprili 28, 2021 jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news