Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today April 25th, 2021

 

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 25/04/2021.

Mikoa Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga: kunatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

.........................

Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi,Lindi, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Mikoa ya Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga na Morogoro, Lindi ,Mtwara, Kilimanjaro, Arusha na Manyara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

............................

Mikoa ya Rukwa, Dodoma, Singida, Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa na Ruvuma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

..............................

KIWANGO CHA JUU CHA JOTO NI NYUZI JOTO 32 ( 32°C ) KATIKA MIJI YA TANGA NA DAR ES SALAAM.

............................

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na Kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 27/04/2021: Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 25/04/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news