Vijana wa kujitolea Jeshi la Kujenga Taifa warejeshwa katika mafunzo

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge, amewarejesha katika mafunzo vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 baada ya kurejeshwa nyumbani mwezi Februari 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma).

Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena akitoa taarifa ya kurejeshwa kwa vijana wa kujitolea katika mafunzo ya JKT kuanzia Mei 7 hadi 14, 2021 baada ya kuwarejesha nyumbani hapo awali.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa wamepangiwa awali kuanzia Mei 7 hadi 14. Amefafanua kwamba vijana waliorejeshwa ni wale wenye elimu ya Darasa la Saba na Kidato cha Nne.

“Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita, Ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada na wale wenye Taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa,” alisisitiza Kanali Mabena.

Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) limekuwa likiendesha mafunzo yakuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali, uzalendo, kilimo, ufugaji na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news