WACHEZAJI 20 WA KMC FC KUWAFUATA DODOMA JIJI KESHO MICHUANO YA ASFC

Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi saba wa KMC FC wataondoka kesho Jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho (ASFC) hatua ya 16 bora utakaochezwa siku ya Jumamosi ya Mei Mosi katika uwanja wa Jamuhuri Jijini humo.
Wachezaji hao wanaondoka Jijini Dar es Salaam wakiwa wameshafanya maandalizi ya kutosha na kwamba kikosi hicho kiko tayari kuwakabili Timu ya Dodoma Jiji katika mtanange huo.

KMC FC chini ya kocha Mkuu John Simkoko, pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo wamejipanga kuhakikisha kwamba licha ya michuano hiyo kuwa na ushindani mkubwa lakini kama Timu itahakikisha kuwa inakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo na hivyo kuendelea katika hatua hiyo ya michuano ya ASFC.

Tunakwenda kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwasababu tunahitaji kupata matokeo mazuri,lakini pia mchezo huo tunauhitaji kwa umuhimu mkubwa sana,kwasababu ukiacha malengo ya kushinda kwenye , lakini pia tunapambana kuchukua kombe hilo msimu huu.

Lakini pia tunawafahamu Dodoma Jiji kuwa ni Timu nzuri natunajua kabisa na wao wamejipanga vizuru hivyo na sisi tumejipanga zaidi kwasababu tunamalengo makubwa kwenye hiyo michuano, lakini pia ni Timu ambayo ipo chini ya Manispaa kama ilivyo KMC FC, watanzania wategemee kuona soka safi kutoka kwa wana Kino Boys.

Imetolewa leo Aprili 28

na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC FC

Post a Comment

0 Comments