WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA KUSAJILI BIASHARA ZAO BRELA

Wafanyabishara na wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kurasimisha biashara zao kwa kusajili majina na alama za biashara zao na kuacha kutumia vyeti vya watu wengine katika kutoa huduma ama kufanya biashara,anaripoti CHRISTINA NJOVU (SONGEA).
Athuman Makuka Msaidizi Usajili alama za biashara na huduma (BRELA) akitoa elimu juu ya namna ya kusajili alama za biashara na huduma kwa wajasiriamali wa viwanda vidogo vidogo Mkoani Ruvuma .
Afisa wa BRELA Rajab Chambega kushoto akimkabidhi cheti cha jina la biashara Ambinga Afrayen Swai mara baada ya kusajili wakati wa utoaji elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na BRELA Mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya utoaji elimu kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyofanyika katika ukumbi wa Sido mjini Songea Afisa biashara wa Mkoa wa Ruvuma Deogratius Sibula amesema kuwa;

“Mkoa wa Ruvuma una wamiliki wa viwanda na biashara wengi, akiwataja baadhi kuwa ni wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vikiwemo viwanda vya unga, wasindikaji wa asali , watengenezaji wa unga wa lishe lakini baadhi yao bado hawaja sajili na wengine kudiriki hata kutumia leseni ama cheti cha usajili cha mtu mwingine” alisema Deogratius.
Washiriki wa Semina ya utoaji elimu kwa umma wakifuatilia kwa makini elimu juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara na leseni inayotolewa na BRELA Mjini Songea.

Aliongeza kuwa wengi wanafanya biashara na hawaja sajili, wengine wanadiriki hata kutumia majina ya bishara ya mtu mwingine na kutolea mfano wa mfanyabishara Wa unga kutumia mifuko ya ama kifungashio chenye nembo na jina la mtu mwingine bila kujua kuwa ni kinyume cha sheria.

Aidha amewataka washiriki kuchangamkia fursa ya kufanya sajili za majina ya bishara zao, kusajili Kampuni , kuhuisha biashara zao na kuona wewe kama mfanyabiashara unasimama wewe mwenyewe katika Biashara yake kwa kufanya usajili na kumiliki jina ama Kampuni yake.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Belinda Lyimo ambaye ni mjasiriamali mchanga ambaye anajishughulisha na usindikaji wa lishe ameishukuru BRELA kwa kufika mkoani Ruvuma na kuwapatia elimu hiyo na kupata pia bahati ya kusajili jina la biashara yeke ambayo inaitwa Belinda Natural Nutritional Products (BNNP) na kupata cheti chake papo kwa papo.
Afisa biashara wa Mkoa wa Ruvuma Deogratius Sibula akimkabidhi cheti bi Belinda Lyimo mara baada ya kusajili wakati wa semina ya utoaji elimu kwa umma juu ya huduma zitolewazo na BRELA.

Belinda ametoa wito kwa wanchi kuchangamkia fursa kwa kwenda kusikiliza elimu mara inapopatikana na kuongeza kuwa yeye binafsi amefurahi sana kwa kuwafikia na isiwe ni mara ya mwisho. 

Nayee Ambinga Afrayeu Swai amewashukuru brela kwa kufika kutoa elimu hii ya usajili wa majina ya biashara na kampuni, hii ni jambo jema kwao wafanyabiashara kwakuwa hii itawawezesha wafanyabiashara kuweka mambo yao sawa ambayo yatawezesha kuweza kutambulika katika mabenki .

Akizungumzia mfumo wa usajili ambao BRELA inautumia wa kufanya sajili kwa njia ya mtandao yaani (ORS) pamoja na changamoto zake mfumo umeweza kusaidia mtu kupata huduma mahali popote ulipo ila vitu muhimu ni kuwa na komputa hata simu katika fanya sajili za majina ya biashara na makampuni. Elimu hiyo kwa umma ambayo ilikuwa ya siku mbili imemalizika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news