Waziri Ummy atamani kuona Tanga Jiji wanajenga maeneo ya michezo ya watoto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Uongozi wa Jiji kuona namna watakavyoongeza kujenga sehemu ya michezo ya watoto katika Jengo la Kitega Uchumi linaloendelea kujengwa Maeneo ya Kange Jijini hapo,anaripoti Nteghenjwa Hosseah (Tanga).
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Jengo la Kitenga Uchumi linalojengwa katika eneo la Kange Jijini Tanga kukagua maendeleo ya mradi huo Aprili 26,2021.

Waziri Ummy alisema kuwa Tanga hakuna maeneo mazuri ya michezo ya watoto kwahiyo ni wakati sasa Jiji la Tanga kuangalia namna mnavyoweza kujenga maeneo hayo ili kuwapa fursa watoto wetu kucheza na kufurahi katika Jiji lao.

Aidha, Mhe. Ummy Mwalimu(Mb) ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la kitega uchumi linaloendelea kujengwa katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Akizungumza katika mradi huo amesema Jengo hilo likikamilika sio tu kwamba litapendezesha mji lakini pia litakua chanzo cha mapato kwa Jiji la Tanga.

“Mradi huu ni wa mfano kwa Halmashauri zingine kuiga na kuanza kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya Halmashauri zao,”aliongeza Waziri Ummy.

Pia aliutaka Uongozi wa Jiji la Tanga kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na thamani ya fedha inaonekana.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Maeji alisema kuwa Mradi huo wa Kimkakati ni jengo la ghorofa moja litakua na huduma za Kibenki, migahawa, maduka, supermarket na maduka ya vinywaji na maeneo ya mama lishe.

Maeji aliongeza kuwa mradi huo mpaka kukamilika utagharimu shilingi Bilioni 8 na utakamilika Nov,2021z

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news