Yanga SC yaichapa Gwambina FC 3-0 dimba la Benjamin Mkapa

Ditram Nchimbi, Bakari Mwamnyeto na Saido Ntibazonkiza wameiwezesha Yanga SC kuondoka na ushindi mnono katika mtanange wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Gwambina FC, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Mtanange huo umepigwa leo Aprili 20, 2021 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Wakati Yanga SC ikiondoka na alama tatu ambazo zimesindikizwa na mabao matatu, wao Gwambina FC kutoka kule Misungwi mkoani Mwanza wamepata bao moja la kufuta machozi kutoka kwa Jimson Mwanuke ndani ya dakika 50.

Yanga SC katika dakika 45 za kwanza waliweza  kutawala mchezo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kisha katika kipindi cha pili Gwambina wasawazisha.

Katika kipindi cha pili ndani ya dakika 59, Ditram Nchimbi alikosa bao la wazi baada ya Kisinda kupiga krosi na Yacouba alipiga pasi ya kichwa kwa Nchimbi ambaye alikosa utulivu na kufyatuka shuti na kupita juu ya goli.
 


Yanga SC ilifanya mabadiliko dakika 66 kwa kumtoa Tusila Kisinda na kuingia Daido Nyibazonkiza, mabadiliko hayo yalitokana baada ya Kisinda kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na tija katika eneo la ushambuliaji katika kupeleka mashambulizi langoni kwa Gwambina.

Mwambusi alifanya mabadiliko mengine dakika 67 kwa kumtoa Yacouba Sogne na kuingia Michael Sarpong kwenda kuongeza nguvu.

Sarpong alionyesha utulivu wa kukaa na mpira kitu ambacho kilikosekana katika kipindi cha kwanza alipokuwa anacheza Yacouba Sogne.

Aidha, dakika 79 Gwambina walipata faulo nje kidogo ya lango la Yanga, Baraka Mtui alipiga faulo hiyo kwa ufundi lakini kipa Faruk Shikhalo aliydaka mpira huo.

Gwambina FC walifanya mabadiliko eneo la kiungo dakika 83 wakimtoa Yusuph Lenge na kuingia Salim Sheshe, wakati huo Gustapha Saimon alionyeshewa kadi baada ha kumfanyia madhambi Kaseke.

Wakati huo huo dakika 85, Yusuph Kagoma alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Kibwana Shomari kwa kumnyooshea mguu juu.

Hata hivyo dakika 94, Saido Ntibazonkiza aligongeana pasi za haraka na Michael Sarpong kisha alionyesha utulivu baada ya kumtoka beki wa Gwambina na kufyatuka shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa na Farouk Shikhalo, Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Dickson Job, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Carlos Carlinhos, Yacouba Songne, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi.
 
Subs: Ramadhan Kabwili, Paulo Godfrey, Bakari Mwamnyeto, Said Juma, Haruna Niyonzima, Michael Sarpong, Saidi Ntibazonkiza.

Gwambina FC kikosi chao kilikuwa na Ibrahim Isihaka, Rajabu Rashidi, Gustapha Saimoni, Baraka Mtui, Novart Lufunga, Yussuph Kagoma, Meshack Mwamita, Yusuf Lwenge, Paulo Nonga, Rajabu Athumani, Japhet Mayungu.

Subs: Mohamed Makaka, Hamad Nassoro, Amos Kidinilo, Salim Sheshe, Mrisho Ngassa, Salum Kipaga, Jimson Mwanuke.
 
Kwa matokeo hayo, Yanga SC inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa alama 57.

 

Post a Comment

0 Comments