Al Ahly ya Misri yatwaa ubingwa wa CAF SUPER CUP

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Al Ahly ya Misri imetwaa taji la Super Cup Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya RSB Berkane katika dimba la Jassim Bin Hamad (Al-Sadd ) mjini Doha nchini Qatar.

Mohamed Sherif ndani ya dakika 57 alionyesha taa ya ubingwa baada ya kuipatia Al Ahly bao la kwanza akimalizia pasi ya Hussein El Shahat.
Ni baada ya kipindi cha kwanza kumalizika ubao ukisoma sufuri pande zote.

Aidha, ndani ya dakika 82, Salah Mohsen aliwatonesha RSB Berkane kidonda baada ya kupachika bao safi akimalizia pasi ya Taher Mohamed ambalo lilikuwa ndilo la mwanzo na mwisho katika mtanange huo.

Hadi dakika tisini, katika michuano hiyo ya CAF SUPER CUP, Al Ahly walikuwa na mabao mawili huku RSB Berkane wakiwa na sufuri, hivyo Al Ahly kutwaa kombe hilo.

Mechi ya Super Cup hukutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa ambaye kwa sasa ni Al Ahly na bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika ambaye ni RSB Berkane.

Post a Comment

0 Comments