BREAKING NEWS: Teddy Mapunda afariki

Habari zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa Teddy Mapunda amefariki dunia muda mfupi uliopita, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.
Kifo chake kinadaiwa kimetokea baada ya kuugua ghalfa wakati akipata futari na wenzake katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan.

Kwa taarifa zaidi Mwandishi Diramakini anaendelea kufuatilia atakujuza hapa.
 
Kuhusu Teddy Mapunda
 
Teddy ni mwasisi wa Kampuni Montage Limited inayojihusisha na masuala ya ushauri na ubunifu nchini Tanzania.
 
Pia ni mbobezi wa miaka mingi katika masuala ya uhusiano wa umma, huduma kwa wateja, utawala, na mauzo.

Teddy Mapunda anakumbukwa kwa kufanya kazi na makampuni mengi ya ndani na nje ya Tanzania ambayo yamepata mafanikio makubwa ikiwemo Serengeti Breweries.

Aidha, Teddy Mapunda ni mhitimu wa Taasisi ya Usimamizi ya Umma ya Uswidi na Taasisi ya Usimamizi na Utawala wa Umma ya Ghana. 
 
Aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Mjumbe wa Bodi ya Kwanini Afrika Sasa ya USA ( Why Africa Now of the USA), TPS Afrika Mashariki (Hoteli za Serena), Taasisi ya WAMA na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Pia itakumbukwa kuwa Machi, 2012, alichaguliwa kuwa mmoja ya wajumbe watano waliounda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB) akiwa Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa Uhusiano Serengeti Breweries Limited.

Teddy amewahi kuwa Katibu Mkuu wa kamati iliyoundwa na TFF ya kusaidia Taifa Star Ishinde mwaka 2015 katika Maandalizi ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia. 
 
RAIS SAMIA AMLILIA TEDDY MAPUNDA

Post a Comment

0 Comments