Dkt.Florence Samizi aibuka kidedea Jimbo la Muhambwe


Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema amemkabidhi cheti cha ushindi aliyekuwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Dkt.Florence Samizi.
Dkt. Samizi ameshinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 23,44I kati ya kura 35,339 sawa na asilimia 68 akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata kura 368.

Post a Comment

0 Comments