🔴LIVE: SIMBA SC vs DODOMA JIJI FC LEO MEI 26, 2021

 Huu ni mtanange wa kusaka tiketi ya kufuzu nusu fainali kati ya Dodoma Jiji FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Awali, Rhino Rangers ikiwa Uwanja wa Kambarage imetolewa katika hatua ya robo fainali kutokana na kichapo walichopata kutoka kwa Azam FC cha mabao 1-3.

Seleman Abdalah alipachika bao kwa Rhino Rangers huku yale ya Azam FC yakifungwa na Ayoub Lyanga, Agreý Morris na Obrey Chirwa.


Azam FC imetinga hatua ya nusu fainali ambapo inamsubiri mshindi wa mchezo wa huu unaoendelea kati ya Simba SC na Dodoma Jiji FC.Timu nyingine zilizofuzu nusu fainali soma hapa.

Matokeo rasmi

Simba SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Nahodha John Raphael Bocco, la kwanza kwa penalti dakika ya 23 na lingine dakika ya 42 wakati la tatu limefungwa na mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere dakika ya 79.

Kwa sasa Simba SC itakutana ma Azam FC iliyoitoa Rhino Rangers ya Tabora leo pia kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Nusu Fainali nyingine itazikutanisha Biashara United na Yanga SC Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora mwezi ujao.

Biashara United waliitoa Namungo FC Jumapili Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara na Yanga wameitoa Mwadui jana FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga wote kwa ushindi wa mabao 2-0

Post a Comment

0 Comments