MAAJABU YA RAIS SAMIA SULUHU KWENYE UONGOZI WAKE

Na Emmanuel J. Shilatu 

Katika kuhakikisha Watanzania wanajivunia na nchi yao, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameweza kuimarisha mahusiano kidiplomasia ya Tanzania kwa nchi jirani na kimataifa. Mfano hai kuimarika kwa mahusiano baina ya Tanzania na Kenya kutokana na pande zote kuondoa vikwazo vidogo vidogo vilivyokuwepo.
Aidha Mhe.Samia ameendelea kuiheshimisha nchi ya Tanzania kimataifa kuwa ni Taifa huru linaloendelea na ukombozi wake wa kiuchumi kupitia miradi ya kimkakati inayoendelea kujengwa nchi nzima. 

Pia ameendelea kuwa mtetezi wa Bodaboda, Wajasiriamali wadogo kwa kuhakikisha Serikali yake inawaheshimu na kuendelea kulinda shughuli zao pasipo kusumbuliwa na mamlaka za mapato na vyombo vya ulinzi na usalama.  

Pamoja na hayo ameendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini na kufanya wawekezaji kukiri hadharani utofauti na maboresho ya kibiashara nchini. 

Mfano hai wa Mwekezaji ni Dangote ambaye ni Mwekezaji wa kiwanda kikubwa cha kutengeneza saruji nchini, ameridhishwa na mazingira ya sasa kuwa hayana urasimu na milango ya biashara yamefunguka sana na yupo tayari kuongeza uwekezaji wa kiwanda kingine kikubwa Tanzania.  

Sambamba na hayo ametoa maelekezo ya yameshatekelezwa ya kufungua akaunti za Wafanyabiashara zilizofungwa kwa sababu mbalimbali na TRA na wakae meza moja na Wafanyabiashara kuona namna bora kumaliza changamoto zilizopelekea akaunti zao kufungwa. Hii imepeleka furaha na vicheko kwa Wafanyabiashara kote nchini. 

Vilevile ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo wanaotuhumiwa na vitendo hivyo amekuwa akiwaweka pembeni na kutoa maelekezo uchunguzi ufanyike. Tumejionea hayo kule bandari, hazina nk. 

Ameendeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa mwendo na kasi ile ile ya awali. Tunajionea miradi ya SGR, Bwawa la Nyerere nk ikiendelea kwa kasi ya ajabu. Huku ni kuenzi kwa vitendo na picha isiyo na shaka ya kuwa kitu kimoja. 

Ukiachana na hayo Rais Samia ameongeza kasi ya ukuzaji ufanyaji biashara nje ya mipaka ya Tanzania. Mfano hai ni furaha na vicheko vya Wafanyabiashara wa Mahindi kwenda nchini Kenya kwa ulaini kabisa kufanya biashara. 

Sanjari na hayo ameendelea kuhakikisha anaimalisha ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka pamoja na kupambana vikali na madawa ya kulevya. Kukamatwa kwa zaidi ya tani ya Madawa ya kulevya kule mkoani Lindi; Mauaji ya Maalbino hayapo; Matukio ya wizi na ujambazi yamepungua kwani walianza kumbipu wakakutana na shoo kali ya Rais Samia. Pongezi za kipekee kwa vikosi vyote vya ulinzi na usalama nchini kwa kazi kubwa wanazoendelea kuzifanya kila siku. 

Hata hivyo Ilani ya uchaguzi 2020 – 2025 inaendelea kutekelezwa vyema kwa vitendo kwa kasi kubwa; Shughuli za Serikali zinaendelea kufanyika pasipo mkwamo wowote ule. Huu ni ushahidi wa kazi kubwa ya ukusanyaji imara wa kodi unaopelekea upatikanaji wa mapato ya ndani yanayowezesha nchi kujitegemea kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news