Mheshimiwa Gekul aipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo umeme vijijini

Na Veronica Simba-REA

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Pauline Gekul, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kutekeleza kazi mbalimbali za maendeleo kwa wananchi ikiwemo miradi ya kusambaza umeme vijijini.
Mheshimiwa Gekul ametoa pongezi hizo asubuhi hii ya Jumatatu, Mei 24, 2021 wakati akitoa salamu katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyika jijini Mbeya.

Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri Gekul amewasisitiza Maafisa Habari kuendelea kutangaza kazi na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kujenga uelewa kwa wananchi ambao ndiyo walengwa wakuu.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa, ambaye amefuatana na viongozi wengine mbalimbali wa Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara husika, Dkt. Hassan Abbas.

Miradi ya kusambaza umeme vijijini hutekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Nishati.

Post a Comment

0 Comments