MWENYEKITI UVCCM TARIME AWATAKA VIJANA KUJENGA UTARATIBU WA KUCHANGIA DAMU, KUFANYA MAZOEZI

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya ya Tarime (UVCCM) Mkoa wa Mara, Godfrey Francis amewataka vijana kuwa na utaratibu wa kujitolea kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wengine pamoja na kupima afya mara kwa mara, anaripoti Amos Lufungulo (Diramakini) Mara.
Amesema, vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wana jukumu la kusaidia kuokoa maisha ya wengine wakiwemo wajawazito,na majeruhi wa ajali kwa kuchangia damu salama pamoja na kupima afya zao ili wajue hatua ambayo itawafanya waishi kwa amani huku wakifanya kazi za uzalishaji mali.

Ameyasema hayo akiwa Mjini Musoma mara baada ya kuchangia damu salama katika Viwanja vya Mukendo ambapo maonesho mbalimbali ya wafanyabiashara, wakulima na taasisi mbalimbali za umma na binafsi zimejumuika kwa ajili ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara uliozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 28, 2021.
 
Pia amesisitiza kuwa, ili maendeleo yafanyike kwa ufanisi lazima wananchi wawe na afya njema.

Ameongeza kuwa, ili Taifa lifikie malengo ya kuwa na uchumi thabiti wananchi lazima wawe na afya njema kwa ajili ya uzalishaji mali kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news