NAIBU WAZIRI WAITARA: OSBP KASUMULU IMEFIKIA ASILIMIA 65

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa mradi wa Kituo cha Huduma ya pamoja kinachojengwa mpakani Kasumulu, wilayani Kyela, mkoani Mbeya umefikia asilimia 65.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo na kuridhishwa na maendeleo yake, Naibu Waziri huyo Waitara amesema kukamilika kwa kituo hicho kutarahisisha taratibu za vibali kwani wadau wote wa usafirishaji watakuwa sehemu moja.

Aidha, ameongeza kuwa kituo hicho cha huduma ya pamoja kitaipa Tanzania fursa kubwa ya kukuza biashara ya mipakani katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

“Kuwaweka wadau wote sehemu moja ni hatua kubwa sana katika utoaji wa huduma kwani walengwa wote watapatikana kwa wakati na kupunguza muda wa kukaa kwenye ofisi na pia kituo kitachangia sana ukuaji wa biashara miongoni wa nchi zetu za kusini mwa Afrika,” amesema Naibu Waziri Waitara.

Naibu Waziri Waitara amemtaka Mkandarasi China Geo Engineering Corporation kuhakikisha wanakamilisha moja ya majengo ili kuruhusu Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutosimamisha huduma kwa kukosa ofisi ya kuhamisha mifumo wanayotumia kwa sasa.
Aidha, amewapongeza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kwa kuhakikisha wataalam wengi wanakuwa wazawa na kuwasisitiza wataalam hao kujifunza ili kuimarisha uzoefu na kujipanga kusimamia miradi mikubwa siku za mbeleni.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daniel Mandari, amesema kuwa kazi za ujenzi kwa sehemu ya majengo yanaendelea kujengwa na fidia kwa wakati waliotakiwa kupisha ujenzi huo wameshalipwa na kupisha ujenzi.

Kaimu Meneja wa TANROADS, Mhandisi Mwita Chacha, amemuhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa kupitia Muwakilishi wa

Wakala huo kuwa kwenye eneo la mradi ni sehemu ya ufatiliaji wa karibu wa ujenzi wa kituo hicho ili kuukamilisha kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Ujenzi wa Kituo hicho unahusisha Jengo la malori, Ghala, jengo la mifugo, jengo la abiria, mageti mawili kwa upande wa Tanzania na Malawi, Tanki la kuhifadhia maji na barabara unganishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news