QUEEN SENDIGA APOKELEWA CCM IRINGA

Na CATHERINE MBIGILI, Iringa

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga ambaye ameteuliwa hivi karibuni kabla ya kuaza kazi amefika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa, kwa lengo la kujitambulisha huku akiahidi kutumia Ilani ya chama tawala katika kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Ilani ya Chama Mkuu wa Mkoa Iringa mpya,Queen Sendiga ,Wakati Wa utambulisho katika ofisi za CCM Mkoa.

Akizungumza baada ya utambulisho huo, mkuu huyo amesema amekuja kushirikiana na wananchi wa Iringa ili kuendeleza yale yaliyofanywa na viongozi waliopita.

Amesema, kitabu cha Ilani ndicho kitakuwa msaafu wake katika utendaji wake wa kazi huku akiahidi kushirikiana na chama katika shughuli zake zote.

"Wote mnafahamu kuwa mimi nimetokea katika chama pinzani ila nina uhakika wote mlisikia hotuba ya mheshimiwa rais aliposema kwamba katika utendaji wake wa kazi hataangalia chama bali ataangalia watendaji pamoja na wale anaoona wana sifa ya kuwatumikia wananchi,"amesema Mkuu wa Mkoa.
Mkuu huyo amesema, amesikia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgomo wa daladala pamoja na migogoro ya ardhi hasa katika wilaya ya Mufindi hivyo aliahidi kuifanyia kazi na kuimaliza kabisa.

Amesema, katika utendaji wake wa kazi amelenga hasa kusikiliza kero za wananchi hivyo muda mwingi atakuwa ni mtu wa kushinda mtaani kuliko ofisini hivyo kama kuna mtu atahitaji kuonana nae ataonana nae akiwa njiani akielekea kazini.

"Nimesikia kuna migogoro ya ardhi ni mikoa mingi inalalamikia tatizo hili, hivyo niwaambie kwamba siyo kwa kuwa imezoeleka kila mkoa kuwa na tatizo hilo basi Iringa tuwe nalo niwatoe hofu kwamba Iringa tunakwenda kulimaliza kabisa,"amesema Queen.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ally Happy akikabidhi ofisi kwa Queen Sendiga ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuutumikia  mkoa wa Iringa.(Picha na Diramakini).

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa, Dkt.Abel Nyamahanga, alimpongeza mkuu huyo kwa kuteuliwa na kumkabidhi Ilani ya chama pamoja na katiba pia aliahidi kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha watu wa Iringa wananufaika na viongozi ili kupata maendeleo.

Amesema, ilani ya Chama Cha Mapinduzi ina mambo mengi ya msingi, lakini ndani ya mambo hayo kuna mambo makuu matatu muhimu ikiwa ni pamoja na kufuta ujinga ,kufuta maradhi pamoja na kuondoa umasikini.

Amesema, chama kimejitahidi kutekeleza mambo hayo kwa kujenga miundombinu pamoja na kuboresha vituo vya afya lengo likiwa ni kumsaidia mwananchi katika kuondokana na mambo hayo matatu.

"Nikuombe sana kiongozi wetu sisi kama chama tutaendelea kukupa ushirikiano katika nia njema ya kuwasaidia wananchi ili utendaji wako uendelee kuwa mzuri,"amesema Mwenyekiti huyo.

Akizungumzia utekelezaji wa chama katika mkoa huo Katibu wa chama,Brown Mwangomale alisema katika mkoa wa Iringa chama kimetekeleza miradi mingi kama miradi ya umeme ,maji,vituo vya afya kila wilaya ila kuna changamoto ndogo za ubovu wa miundombinu ya barabara hasa katika wilaya ya Kilolo na migogoro ya aridhi katika wilaya ya Mufindi.

Amesema, wanaimani kiongozi huyo waliyoletewa ataenda kuzifanyia kazi huku chama nacho wakitoa ushirikiano ili kumaliza kabisa changamoto hizo.

Amesema, moja ya mafanikio makubwa yaliyopo Mmkoani hapa ni umeme na maji ambavyo vipo kwa utoshelevu na hakuna siku ambayo viliwahi kutolewa kwa mgao kama wanavyoshuhudia katika mikoa mingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news