Rais Samia atengua teuzi, ateua

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Camilius Wambura kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
Aidha, pamoja na kumpandisha cheo,Rais Samia amemteua CP Camilius Wambura kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Kabla ya uteuzi huo, CP Wambura alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi (CP).

Licha ya kumpandisha cheo, Mhe. Rais Samia amemteua CP Hamad kuwa Mkuu wa Kamisheni ya Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, CP Hamad alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Katika hatua nyingine,Rais Samia ametengua uteuzi wa Azza Hilal Hamad aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Bi. Azza atapangiwa majukumu mengine.

Kufuatia uamuzi huo,Rais Samia amemteua Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.

Kabla ya uteuzi huo Kayombo alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango na ataapishwa pamoja na Makatibu Tawala wengine Juni 2, 2021 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news