Rais Samia ateua mabalozi 23

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Bi.Hoyce Temu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Mei 22, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imewataja mabalozi hao wapya kuwa ni Luteni Jenerali Yakub Mohamed, Meja Jenerali Richard Makanzo, Pereira Ame Silima, Maulidah Hassan na Togolani Mavura.

Wengine ni Edwin Rutegaruka, Fredrick Kibuta, Noel Kaganda, Mindi Kasiga, Caroline Chipeta, Macocha Tembele, Agnes Kayola, Masoud Balozi, Ceasar Waitara, Swahiba Mndeme pamoja na Said Mshana.

Pia Rais Samia amewateua Alex Kallua, Mahmoud Kombo, James Bwana, Said Mussa, Elsie Kanza pamoja na Robert Kahendaguza.

“Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza leo Mei 22, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye,” imesema taarifa hiyo kama inavyoendelea kusomeka hapa chini;Post a Comment

0 Comments