Meya, DED Kinondoni wanusurika kutumbuliwa, RC ayamaliza

Na Diramakini (diramakini@gmail.com).

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza kati ya meya Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa, Spora Liana.
Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.
 
Hatua hiyo inafikiwa baada ya hivi karibuni viongozi hao wawili kutofautiana kutokana na makusanyo ya fedha za ushuru wa taka ndani ya halmashauri hiyo.
 
Awali, Mkurugenzi huyo alidai kuwa, kuna kasoro katika ukusanyaji wa fedha hizo kwani, baadhi ya watendaji ambao si waaminifu huwa wanatoa sitakabadhi za malipo zenye viwango vidogo tofauti na walizotozwa kwa ajili ya huduma ya uzoaji wa taka.

Post a Comment

0 Comments