Shemsha Mohamed Seif aibuka kidedea Mwenyekiti CCM Simiyu

Mwanamama mpambanaji na jasiri katika siasa, Shemsha Mohamed Seif amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Simiyu, anaripoti Derick Militon (Diramakini) Simiyu.

Shemsa Mohamed Seif . Picha na Diramakini (diramakini@gmail.com).

Shemsha ameibuka mshindi kwa kura 441 kati ya kura 704 zilizopigwa huku Alphonce Burugu akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 174 na Sakina Omary akishika nafasi ya tatu kwa kura 89.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo kufariki dunia asubuhi ya Jumanne Februari 23, 2021 nyumbani kwake Mwanuzi wilayani Meatu.

Post a Comment

0 Comments