TARI yataja sababu za kilimo cha pamba kutokubali mkoani Dodoma

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) imebainisha kuwa sababu za kilimo cha zao la pamba kutokubali katika mkoa wa Dodoma baada ya kuanzishwa miaka miwili iliyopita katika wilaya za Chemba, Bahi na Chamwino ni kutokana na changamoto za hali ya hewa ambazo haziendani na kilimo cha zao hilo.
Picha zikiwaonesha washiriki wa maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu ambapo TARI inashiriki kuonesha namna teknolojia inavyotumika kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. (Picha zote na TARI).
Mwishoni mwa mwaka 2018 bodi ya pamba chini ya wataalamu wake walizunguka katika wilaya hizo kuwahamasisha wananchi kulima Pamba.

Hata hivyo matokeo hayakuwa mazuri licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wananchi ambapo TARI inaeleza kuwa changamoto ya hali ya hewa ikiwamo ikolojia ya mkoa wa Dodoma kutoendana na kilimo cha zao hilo.
Mkurugenzi mkuu wa TARI, Dkt.GEOFRY MKAMILO amebainisha hayo katika viwanja wa Jamhuri yanapoendelea maonesho ya kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu ambapo Taasisi inashiriki kuonesha namna Teknolojia inavyotumika kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini.

Kwa mwaka wa Pili sasa TARI imekuwa na Idara maalum usambazaji Teknolojia ambapo inajivunia kutumia idara hiyo kusambaza teknolojia kwa wakulima nchini kupitia kwa maafisa Ugani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news