TBS YAWATAKA WAUZAJI WA BIDHAA KUONDOA SOKONI AMBAZO ZIMEKWISHA MUDA WAKE

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na ukaguzi wa bidhaa Kanda ya Ziwa ambapo limefanya ukaguzi katika maduka ya chakula pamoja na viwanda vya kuzalisha mifuko ya sandarusi jijini Mwanza.
Mkaguzi wa TBS Kanda ya Ziwa Bw.Donald Mkonyi akiangalia ukomo wa matumizi ya bidhaa katika duka la chakula wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni katika Halmashauri ya Nyamagana. Wauzaji walisisitizwa kuziondoa sokoni mara moja bidhaa zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa afya za walaji.

Wazalishaji wameshauriwa kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango ili kuweza kumlinda mteja.

Wakati huo huo wauzaji wa bidhaa wametakiwa kuhakikisha wanaziondoa sokoni mara moja bidhaa zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa afya za walaji.
Wakaguzi wa TBS kanda ya ziwa wakiwa katika ukaguzi wa kushtukiza katika viwanda vya kuzalisha mifuko ya sandarusi vilivyopo jijini Mwanza kwa ajili ya kuangalia uzalishaji pamoja na uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya kupima maabara kama zimekidhi matakwa ya kiwango husika.

Post a Comment

0 Comments