UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 15/05/2021

Mikoa ya Kagera na Mara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Geita, Mwanza na Simiyu: inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

...............................

Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

................................

Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Pwani,(ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Morogoro, Mtwara, Lindi, Ruvuma,

Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Dar es Salaam na Tanga: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

................................


KIWANGO CHA JUU ZAIDI CHA JOTO NI NYUZI JOTO 31 ( 31°C ) KATIKA MIJI YA DAR ES SALAAM, TANGA, KILWA, KIBAHA, PAMOJA NA KISIWA CHA UNGUJA.

..................................

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa Kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumatatu tarehe 17/05/2021: Mabadiliko Kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 15/05/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news