Wahamasishwa kuzalisha bidhaa zenye ubora

Wajasiriamali kote nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya SIDO Kanda ya Kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa Babati mkoani Manyara.

Naye Meneja wa Uthibiti Ubora wa TBS Bw.Gervas Mwanjabala akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya TBS kutoa elimu ya masuala ya viwango kwa wajasiriamali waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali nchini na vilevile n fursa ya kusikiliza maoni na changamoto za wajasiriamali na wananchi kwa ujumla na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

“Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao”. Amesema Bw. Mwanjabala.

Aidha Meneja wa kanda ya kaskazini wa TBS, Bi. Happy Brown aliwataka wajasiriamali wote katika kanda hiyo kutosita kutoa taarifa zozote ili waweze kusaidiwa na hata kupatiwa ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaaa bora.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS Bi. Deborah Haule amesema muitikio wa watu katika maonesho haya umekuwa mkubwa na wajasiriamali wengi wamejitokeza kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na taratibu za kufuata ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Amesema wajasiriamali wadogo nchini hawaingii gharama zozote bali wanatakiwa kupitia SIDO ili watambulike na wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi. Deborah amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news