Wajasiriamali wapewa mbinu za kuyafikia malengo ya haraka kiuchumi

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Wajasiriamali hapa nchini wametakiwa kuhakikisha kwamba wanazalisha bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutafuta masoko ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa Elimu ya Masoko ambaye pia ni Mkurugenzi wa Veva Craft, Genoveva Mtiti wakati akitoa mada katika mafunzo ya Wajasiriamali yaliyofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Arizona kilichopo Mikocheni A mkoani Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Veva Craft pamoja na Chuo cha Ufundi cha Arizona.

Mtiti amesema, wajasiriamali wengi wamekuwa wakizalisha bidhaa bila Kuzingatia ubora na muonekano wa nje wa bidhaa na hivyo kuishi kuzalisha bidhaa zinazoshindwa kuingia katika soko kubwa na wanaishia kubaki na bidhaa ndani na kuishia kuuza mitaani kwao tu.

Wajasiriamali zaidi ya 50 kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam walishiriki mafunzo hayo ambapo Mtiti aliwataka kuhakikisha kwamba kabla ya kutimia mitandao ya kijamii kutafuta masoko wahakikishe bidhaa wanazozalisha zinakuwa katika ubora unatakiwa.

"Wajasiriamali wengi wanazalisha bidhaa nyingi Sana lakini tatizo linakuja kwenye namna ya kupaki au kuweka rabo kwenye biashara zao na hivyo muonekano wa nje kutomvutia mteja.

Anaendelea kuwa mjasiriamali anapaki bidhaa yake ili mradi tu, kama uko makini na biashara yako jitahidi kuhakikisha bidhaa, kifungashio hadi rebo vyote vina mvutia mteja na anashawishika kununua.

Amesema si kazi ngumu wa rahisi Sana kutafuta masoko kwenye mitandao ya kijamii lakini kama wanataka kufanya biashara wanaweza na kwa kutumia mitandao hiyo watafanikiwa.

Amesema masoko yako mengi Sana Ila wanachotakiwa kufanya kwanza ni kutafiti hitaji la walaji pamoja na kutangaza bidhaa zao bila kuchoka.

Aidha amewataka Wajasiriamali hao kuwasiliana naye pale wanapo kumbana na changamoto zozote hususani katika masuala ya masoko na mambo mengine ya kitaalamu.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya masoko na ushauri wa kitaaluma ni kwa jinsi gani bidhaa za Wajasiriamali wadogo zinaweza kuboreshwa kufikia viwango bora ili kuingia sokoni kwa urahisi na kukabiliana na ushindani sokoni.

Naye, Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arizona, Jenifar Shigoli aliwasisitiza Wajasiriamali hao kutochoka kutafuta maarifa na badala yake kutumia Chuo hicho ambacho kina wataalamu mbali mbali wa uzalishaji wa bidhaa.

Kwa upande wao Wajasiriamali hao waliwashukuru waandaaji wa mafunzo hayo ambayo wamesema yatawasaidia katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za masoko hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments