Waliohitimu Kidato cha Sita mwaka 2021 waitwa mafunzo ya JKT

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Leo Mei 22, 2021 vijana waliohitimu elimu ya sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2021 wametakiwa kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria kuanzia Juni 10, hadi Juni 10, mwaka huu.

Kaimu Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kanali Hassan Mabena amesema, jeshi hilo tayari limewapangia makambi vijana hao katika kambi za JKT Rwamkoma Mara,JKT Msange Tabora,JKT Ruvu Pwani,JKT Mpwapwa,Makutupora JKT Dodoma,JKT Mafinga Iringa na JKT Mlale Ruvuma.

Aidha, kambi nyingine zilizopangwa ni JKT Itaka Songwe,JKT Luwa,JKT Milundikwa Rukwa ,JKT Nachingwea Lindi na JKT Kibiti Pwani na Oljoro JKT Arusha ,JKT Mgambo,JKT Maramba Tanga,JKT Makuyuni Arusha ,JKT Bulombora na JKT Mtabila Kigoma.

“Jeshi la kujenga taifa JKT linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 1 hadi 10 june 2021,” amesema Kanali Mabena.

Aidha, Kanali Mabena amesema kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya JKT Ruvu Pwani kwani ni kambi yenye miondombinu kwa watu wenye ulemavu na wanauwezo wa kuhudumia watu kama hao.

Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa kama bukta ya dark bluu yenye mpira kiunoni na yenye mifuko mirefu na yenye zipu, T shert ya rangi ya kijani, raba za michezo zenye rangi ya kijani na blue, shuka mbili za kulalia zenye rangi la blue bahari.

Vifaa vingine ni Soksi ndefu za rangi nyeusi, nguo za kujikinga na baridi kwa waliopangiwa kwenye mikoa yenye baridi, track suti ya rangi ya kijani au blue, nauli ya kwenda na kurudi nyumbani, Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za Maisha na utayari wa kulijenga taifa na kulitumikia taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news