WAMILIKI WA KAMPUNI ZA BIASHARA HAPA NCHINI WAASWA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja ametoa wito kwa Wafanyabiashara na wamiliki wa Makampuni mbalimbali hapa nchini kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini kupitia biashara zao, ANARIPOTI JOHN BERA (WMU) Mwanza.

Mhe. Mary Masaanaja ametoa wito huo leo Jijini Mwanza, wakati wa maonesho ya Biashara ,Uwekezaji na Utalii yanayowahusisha wadau mbalimbali. Amesema wafanyabiasha ni wadau wakubwa wa utalii hivyo wana nafasi kubwa ya kuutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya Watalii.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akiwaasa wamiliki wa Kampuni za Biashara nchini kutumia fursa hiyo kuutangaza Utalii wakati wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika leo jijini Mwanza.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja kabla ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika Jijini Mwanza.

“Nawaomba sana ninyi wafanyabiashara, kupitia makampuni yenu mtangaza Utalii wa Tanzania na vivutio vyake ,ninyi ni wadau wakubwa wa utalii,"amesema Mhe. Mary Masanja.

Amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa kutambua kuwa Sera ya Tanzania ya Viwanda itaendelea kutekelezwa kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekua akiwasisitiza Watanzania wawekeze katika miradi mbalimbali ya maendeleo “
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Nchemba akipokea vitabu kutoka kampuni ya Global Education Link kabla ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yaliyofanyika leo jijini Mwanza. pembeni yake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Massanja akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo amesema wafanyabiashara wakishirikiana vizuri wataweza kukuza uchumi wa nchi pia kuutangaza utalii.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ikiwemo uondoaji wa urasimu na ukiritimba kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini.

“Serikali tunaendelea kuziondoa changamoto kuziondoa changamoto zote zinazolalamikiwa na wafanyabiasha na wawekezaji,tuvute subira kidogo haya mambo yatakwenda kurekebishwa vizuri,“amesema Mhe. Mashimba.

Hatahivyo, amezitaka Mamlaka za Serikali za mitaa kutengeneza wafanyabiashara watakaolipa mapato kwa kuwapatia maeneo watakayo fanyia Biashara Ili waweze kulipa kodi na kukuza uchumi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments