Waziri Bashungwa ampongeza Waziri Jafo kwa kuwashirikisha wadau wa sekta yake

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashunwa ametoa Shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe. Suleman Jafo kwa kuwateuwa Wasanii na Wanahabari kuwa Wajumbe na Mabalozi wa Mazingira wa Kamati Maalumu ya Mazingira Watakaoshiriki katika Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira Nchini.

“Mhe Waziri Jafo ninakushukuru na kukupongeza kwa kuwashirikisha wadau wetu katika tasnia ya sanaa, habari na michezo katika wajumbe wa kamati maalum na mabalozi wa mazingira watakaoshiriki kuhamasisha na kuwezesha ushiriki wa jamii na wadau katika kampeni za utunzaji mazingira.

“Ninawashukuru wote walioteuliwa kwa kupokea jukumu hili, sina shaka kila mmoja wenu atalifanya kikamilifu. Huu ni mmoja wa mfano mzuri wa namna ya kutumia tasnia za habari, sanaa na michezo kunufaika binafsi kwa upande wa wadau, lakini sanjari na lengo hilo, kusaidia maendeleo ya jamii na nchi.

“Natoa ombi kwa wasanii, wanahabari, wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri wakuu, wanamichezo, na wadau wote kuunga mkono kauli mbiu ya kampeni ya utunzaji mazingira isemayo: MAZINGIRA YANGU, TANZANIA YANGU NAIPENDA DAIMA,”ameeleza Waziri Bashungwa.

Wajumbe hao Walioteuliwa Baadhi ni Ben Paul (Mwanamuziki), Mwasiti Almasi (Mwanamuiki), Steve Nyerere (Msanii/Mwigizaji), Oliver Nyalinga (Mwandishi), Zuwena Mohamed/Shilole (Mwanamuziki/Mwigizaji), Bw. Maulid Kitenge (Mtangazaji), Yvone Cherrie/ Monalisa (Mwigizaji), Haji Manara (Msemaji wa Timu ya Simba), 

Antonio Nugaz (Afisa Uhamasishaji Yanga), Aneth Andrew (Mwandishi), Nancy Sumari (Miss Tanzania), Millad Ayo (Mtangazaji), Charles Hillary (Mtangazaji), Bakari Kafuti/Beka Flavor (Mwanamuziki), Rajabu Abdul/Harmonize (Mwanamuziki), Christina Shusho (Mwanamuziki), Mrisho Mpoto (Mwanamuziki), Ally Kiba (Mwanamuziki), Baby Kabae (Mtangazaji), Nassib Abdul/Diamond Platnumz (Mwanamuziki), Faustina C. Mfinanga/Nandi (Mwanamuziki)

Post a Comment

0 Comments