WAZIRI CHAMURIHO KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema atafanya ukaguzi wa kushtukiza katika Taasisi zilizo chini ya Wizara yake lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi katika taasisi hizo, ANARIPOTI SITI SAID (WUU).

Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Wafanyanyakazi wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Waziri huyo amesema kuwa ukaguzi huo utaenda sambamba na kufanya mabadiliko ya uongozi na Wafanyakazi wa Taasisi hizo endapo utendaji wao utakuwa hauridhishi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Malongo (kulia), katika kikao cha baraza hilo, jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi kujadili mpango na makisio ya Bajeti ya Sekta hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22, jijini Mwanza.

“Kuna Taasisi ambazo zimekuwa na malalamiko ya hapa na pale, kwa sababu Wizara ni sikivu tumeyasikia, na tutapita kufanya ukaguzi katika Taasisi hizi, endapo tutakuta watendaji wa Taasisi hizi wanafanya ndivyo sivyo, hatutasita kufanya mabadiliko stahiki ili tuendane na matarajio ya watanzania wote”, amesema Chamuriho.

Aidha, amewataka watumishi wa Sekta hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, juhudi, maarifa, maadili ya fani husika na maadili ya Utumishi wa Umma ili kuleta utendaji wenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Chamuriho ametoa wito kwa Menejimenti ya Wizara na Taasisi zote za Wizara, kuhakikisha thamani ya fedha na ubora katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miradi ya ujenzi inaonekana wazi wazi na kuzingatiwa kwa mujibu wa vigezo na viwango vilivyowekwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Sekta hiyo, Mhandisi Joseph Malongo, akitoa taarifa ya utendaji wa Sekta kwa wajumbe wa baraza hilo, jijini Mwanza.
Amebainisha kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha ukaguzi wa ubora wa barabara na viwanja vya ndege ikiwa ni pamoja na kutumia mitambo maalum ya ukaguzi ili kuokoa matumizi ya fedha nyingi za Serikali na kuongeza ubora wa miradi yote ya ujenzi nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Sekta hiyo, Mhandisi Joseph Malongo, amesema kuwa Kikao hiko kitajadili masuala mbalimbali ya watumishi kwa nia ya kutimiza lengo la kuboresha ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi mahali pakazi.

Ameongeza kuwa Wizara kupitia Sekta hiyo inaendelea na jitihada za kudhibiti ubora wa usimamizi wa ujenzi wa miradi ya barabara, majengo, madaraja, vivuko, huduma za ufundi na umeme pamoja na viwanja vya ndege lengo ni kuhakikisha viwango vya ujenzi vinafikiwa na pia kupunguza gharama za miradi.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (hayupo pichani), wakati walipokutana ili kujadili mpango na makisio ya Bajeti ya Sekta hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22, jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, katika picha ya pamoja na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi lililolenga kujadili mpango na makisio ya Bajeti ya Sekta hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22, jijini Mwanza. (PICHA NA WUU).

Naye, Katibu wa Baraza hilo, Wakili Fanuel Muhoza, akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Sekta hiyo amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, uadilifu pamoja na weledi ili kuhakikisha Sekta hiyo inafikia malengo yake iliyojiwekea.

Mkutano huu wenye ajenda ya kujadili Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 umeshirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Wizarani na Taasisi mbalimbali za Sekta hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news