Waziri Kalemani awasimamisha kazi watumishi TANESCO kero ya LUKU

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Waziri wa Nishati Mh.Dkt.Medard Kalemani ameagiza kusimamishwa kazi kwa siku 10 watumishi watatu wa TANESCO akiwemo Meneja wa mfumo wa LUKU kwa kushindwa kutatua tatizo la LUKU lililojitokeza kwa siku tatu na kuleta usumbufu kwa wananchi.
Waliosimamishwa kazi ni Meneja wa TEHAMA na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na Wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki na kusema endapo maelezo yao hayatojitosheleza wataondolewa kazini.

Kwa muda wa siku tatu, Wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Kielekroniki hivyo kulilazimu Shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za Mikoa na Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news