WAZIRI MWAMBE ATOA SIKU 14 KWA WAWEKEZAJI KUWASILISHA KERO ZAO

NA EMMANUEL MBATILO, Dar es Salaam

Waziri wa Uwekezaji Mhe.Geofrey Mwambe ametoa siku 14 kwa wawekezaji nchini ambao shughuli zao za uwekezaji zimesimama au zimekwazwa kutokana na maamuzi ya taasisi za Serikali kuandika barua na kuzipeleka wizarani ili kuweza kushughulikiwa.
Waziri wa Uwekezaji Mhe.Geofrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uwekezaji Mhe.William Ole Nasha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) leo Jijini Dar es Salaam.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kuzungumza na waandiahi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Mhe.Mwambe amesema “Kuna wawekezaji ambao wamekuja na kuanguka hawakufanikiwa kuweza kupata idhini ya kuwekeza hivyo hawa wawekezaji wote waje waandike barua kwetu tutakaa ndani ya wizara tutajadiliana na kuona ni namna gani ya kuwasaidia kutoka pale walipokwama kwenda mbele”. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.Maduhu Kazi akizungumza katika kikao cha Waziri wa Uwekezaji na Watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) leo Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mwambe amesema kuwa sekta binafsi inamadhaifu mengi hivyo amewataka wawe wamoja kwa kushirikiana ili kukuza uwekezaji hapa nchini.

“Sekta binafsi acheni kutoa Rushwa hivyo mjikite zaidi katika ulipaji kodi ili kuweza kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini”. Amesema Mhe.mwambe.

Pamoja na hayo Mhe.Mwambe ameziomba taasisi za Serikali kushirikiana kuyajenga makampuni ya kitanzania yaliyosajiliwa na kufanya kazi hapa nchini ili kuwasababishia wapate faida na serikali ipate fedha nyingi.

Hata hivyo, Mhe. Mwambe amewaonya baadhi ya wafanyabiashara kuwatumia maafisa wa serikali kuwakandamiza wawekazaji wengine ambao wanakuja Tanzania kuwekeza hivyo wakizidi kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news