Amteka mpenzi wake na kumuua

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya ya Bukombe mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.
Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari amesema kwamba, mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake Juni 13, mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu.

Kamanda Mwaibambe amesema, baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana, lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe,"amesema Kamanda Mwaibambe.

Aidha, amesema mtuhumiwa aliwaongoza askari polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news