AY akubali kuwa balozi kijiji cha wasanii Mkuranga

Na Peter Mwenda

MWANAMUZIKI nguli wa kizazi kipya Ambwene Yassayah (AY) ameahidi kuwarudisha wanamuziki wenzake kama balozi mpya wa wasanii wa fani mbalimbali kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Babu Chilo kushoto akiwa na AY.

Mwanamuziki huyo aliyewawakilisha Joseph Haule (Profesa J), Fareed Kubanda (FED Q), Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) alisema kijiji cha wasanii kitawakomboa wasanii wakiwekeza Kijijini.

"Mimi na wasanii wenzangu tulikuwa waanzilishi wa kijiji hiki (2010) miaka kumi iliyopita tulijisahau lakini sasa tunarudi kwa nguvu zote kuhakikisha yale tuliyoyaanzisha tunayasimamia"alisema AY.
Wachezaji wa kijiji cha wasanii Mwezenga.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga, akizungumza baada ya mwanamuzi AY kutambulishwa ofisini kwake, aliahidi kutimiza ahadi kwa kijiji cha wasanii Mwanzega kwa kuboresha miundombinu ya barabara, Umeme na maji salama.

Sanga aliahidi ukamilishaji huo mbele ya Mkurugenzi wa wilaya Injinia Mshamu Munde ambaye kwa upande wake alisema wilaya itahakikisha inatoa ushirikiano kwa wasanii pamoja na jamii inayozunguka kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya alipokea jezi za Simba na Yanga zitakazotumiwa na vijana wa kijiji cha wasanii.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga akizungumza baada ya mwanamuzi AY kutambulishwa ofisini kwake Mkuu wa WIlaya Philberto Sanga aliahidi kutimiza ahadi kwa kijiji cha wasanii Mwanzega.

Alisema michezo ni Afya hivyo anampongeza mwanachama Issere Sports kwa kutoa vifaa hivyo vya michezo vitakavyotumika katika kijiji hicho na akawata wadau wengine wa michezo kusaidia kijiji hicho.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii nchini (SHIWATA), Deo Kway alisema mtandao huo umeanza kutoa maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya wawekezaji wa sanaa mbalimbali.

Deo alisema SHIWATA mbali ya wasanii wanachama wakamilishe ujenzi wa nyumba zaidi ya 250 na ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kuingiza watu 2,000 kwa pamoja baada kukabidhiwa ramani ya ukumbi huo.

Msanii maarufu Ahmed Olotu ( Babu Chilo) aliwashauri wasanii wanachama wa SHIWATA waliofanikiwa kimaisha warudi kuwekeza Kijijini kujenga hosteli za wasanii wapate mafunzo kuandaa chipukizi wapya wa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news