HABARI KATIKA PICHA: MKUTANO WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO JUNI 21, 2021

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, jaji (mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana (aliyekaa katikati) akisaini nyaraka wakati wa Mkutano wa Tume Na. 4 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ulioanza leo Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mheshimiwa George Yambesi , Kamishna wa Tume (kushoto) na Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma. (Picha na PSC)
Baadhi ya Maafisa wa Tume wakifuatilia Mkutano wa Tume Namba 4 kwa mwaka 2020/2021 ulioanza leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Bibi Neema mkenda (Afisa Utumishi), Bibi Kombe Shayo (Katibu wa Afya) na Bibi Christina Muhe (Afisa Utumishi). (Picha na PSC).
KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji (aliyesimama) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Tume namba 4,kwa mwaka 2020/2021 Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kamishna wa Tume, Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay. (Picha na PSC).
MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2021: Mkurugenzi wa Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Bambumbile Mwakyanjala (kulia) akifafanua jambo kwa Maafisa wa Tume wanaoshirika katika kupokea kero, malalamiko na changamoto za kiutendaji kutoka kwa Watumishi wa umma, leo katika Ofisi ya Tume Mtaa wa Luthuli Jijini dar es Salaam. (Picha na PSC).

Post a Comment

0 Comments