KANDA YA ZIWA YATAMBA FAINALI ZA UMITASHUMTA

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Wanariadha kutoka mikoa ya kanda ya ziwa yaani mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga na Simiyu wamejizolea kwa wingi nafasi ya mshindi wa kwanza hadi wa tatu katika mashindano ya UMITASHUMTA yanayofikia tamati kesho.

Ukiacha wanariadha wa kutoka mikoa ya Manyara, Lindi, Singida, Tabora, Arusha na Singida, zawadi nyingi zimeenda kwa wanariadha kutoka kanda ya ziwa.

Wanariadha kutoka kanda ya ziwa wametamba katika mashindano ya mbio za mita 100 kwa wavulana, mita 200, mita 400, mita 800 na mita 1500.
Katika mbio za mita 100 kwa wavulana, mshindi wa kwanza ni Kimana Kibase kutoka mkoa wa Simiyu ambaye alitumia sekunde 12:09 na kufuatiwa na mwanariadha Siprious Pius wa Mara ambaye alikimbia kwa kutumia sekunde 12: 22 na wa tatu Pascal Norbet alikimbia kwa kutumia sekunde 12:81.

Mshindi wa mbio za mita 100 wasichana anaitwa Coletha Antony wa Lindi ambaye alitumia sekunde 13:60 na kufuatiwa na Jesca Leonard wa Arusha aliyetumia sekunde 13:72, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mwanariadha Hamisa Mkwande wa Singida aliyekimbia kwa sekunde 13:75.

Katika fainali za mbio za mita 400 kwa wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanariadha Samweli Yohana wa Singida alishinda mbio hizo akitumia sekunde 56:18, nafasi ya pili ikichukuliwa na Papius Charles wa Kagera aliyekimbia kwa sekunde 57:50 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Emanuel Nyamagaini wa Mara ambaye alitumia sekunde 58:03.
Aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wasichana katika mbio za mita 400 anaitwa Sharifa Mauzo wa Lindi ambaye alikimbia kwa dakika 1:03:56, ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Martha Muhinda wa Mwanza ambaye alitumia dakika 1:03:88, na nafasi ya tatu ilikwenda kwa mwanariadha Lightnes Msemwa wa Iringa ambaye alitumia dakika 1:04:41.

Katika mchezo wa fainali za mbio za mita 800 wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanariadha Ashraka Katambo wa Lindi ambaye alitumia muda wa dakika 2:10:63, nafasi ya pili ilichukuliwa na Augustino Noni wa Kagera aliyetumia dakika 2:10:78 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Michael Paulo wa Mara aliyetumia muda wa dakika 2:10:84.

Msichana aliyeshika nafasi ya kwanza mbio za mita 800 anaitwa Salma Samwel wa Shinyanga ambaye alitumia muda wa dakika 2:26:06, nafasi ya pili ilichukuliwa na MilembeMathias wa Mwanza aiyetumia dakika 2:26:72 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Roisi Manyama wa Mara ambaye alitumia dakika 2:10:84.

Katika fainali za mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 100 kwa wavulana, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na wanariadha wa mkoa wa Mwanza, na kufuatiwa na Mara na mkoa wa Geita ulishika nafasi ya tatu.

Kwa upande wa wasichana, mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 100 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na wanariadha wa mkoa wa Dar es salaam, nafasi ya pili ilichukuliwa na mkoa wa Mwanza huku wanariadha wa mkoa wa Morogoro wakishika nafasi ya tatu.

Katika fainali ya mbio nyingine za kupokezana kijiti 4 x mita 400 nafasi ya kwanza kwa wavulana ilichukuliwa na mkoa wa Mwanza, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mara huku nafasi ya tatu ikishikwa na mkoa wa Kagera.

Kwa wasichana mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 400 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Mwanza, mkoa wa Mara ulishika nafasi ya pili huku Tabora ikishika nafasi ya tatu.

Katika mchezo wa kurusha kisahani kwa wavulana nafasi ya kwanza alishinda Daudi Jumanne wa Geita ambaye alirusha umbali wa mita 30, akifuatiwa na Mohamed Athumani wa Mara ambaye alirusha umbali wa mita 26 huku Awadh Omary wa Tanga akirusha umbali wa mita 26.

Kwa wasichana nafasi ya kwanza katika mchezo wa kurusha kisahani ilishikwa na Tatu Miraji wa Pwani aliyerusha umbali wa mita 20, Solile Gayi wa Mwanza alirusha umbali wa mita 19 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Anna Samweli wa Mara aliyerusha umbali wa mita 19.

Katika Fainali maalum za mpira wa goli Tanga wasichana wameifunga Morogoro magoli 8-7 na kwa upande wa fainali ya mpira wa goli wavulana Morogoro imeifunga Rukwa magoli 13-4.

Katika mchezo wa fainali wa soka maalum Njombe imeifunga Dar es salaam magoli 2-1.

Katika mchezo wa kugombea nafasi ya tatu wavulana kati Mara na Katavi matokeo ni Mara imeifunga katavi magoli 3-0, na kwa wasichana Katavi imeifunga Manyara magoli 3-0.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news