Katibu Mkuu Mhandisi Sanga atoa maagizo kwa wataalam wa mifumo ya Ankara za Maji

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amewataka wataalamu wa TEHAMA wa Wizara hiyo kuhakikisha wanaandaa Mazingira ya uhakika ya miundombinu ya TEHAMA ili mfumo wa pamoja wa kusimamia huduma za ankara za Maji kwa Mamlaka za Maji nchini uwe unapatikana saa 24 kwa siku zote 7 kwa wiki kwa mwaka mzima. Amesema mfumo huo umeonesha manufaa kwa Mamlaka ambazo zimeanza kuutumia kutokana na kuondoa changamoto nyingi ikiwemo gharama na usalama wa taarifa za wateja.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na watalamu wa mifumo Mfumo wa pamoja wa Ankara za Maji (hawapo Pichani).

Ametoa kauli hiyo Juni 11, 2021 wakati wa kufunga mafunzo yaliyolenga kutoa uelewa wa pamoja juu ya kusimamia huduma za ankara za wateja wa Maji yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutamno wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Tabora.

Amesema mfumo huu ni wa uhakika na ni salama kwa Serikali kwa sababu umetengenezwa na wataalamu wa Serikali kupitia Wakala wa Serikali Mtandao na unakidhi mahitaji ya serikali kwa sasa.
Baadhi wa wajumbe wa mafunzo ya mfumo wa Pamoja wa kusimamia ankara za maji wakiendelea na kikao.

“Mifumo mingine iliyopo kwenye Mamlaka za Maji nchini kwa asilimia kubwa inamilikiwa na Wakandarasi au Wataalamu Washauri. Kwa hali hiyo Wakandarasi au Wataalamu Washauri waliotengeneza Mifumo hiyo ndio wenye kumiliki taarifa za Wateja na wakati mwingine taasisi haiwezi kuandaa Ankara za Malipo bila kuwasiliana na Wakandarasi hao kinyume na matakwa ya Serikali. Kwa mantiki hiyo kama Wizara na Sekta ya Maji kwa ujumla tumeamua kutengeneza Mfumo huu Jumuishi wa Kusimamia Ankara za Maji ili kuepukana na changamoto hiyo, hivyo wataalamu wa TEHAMA mna jukumu la kuhakikisha mfumo unakuwepo muda wote,"amesema Mhandisi Sanga.

Amesisitiza Kuwa mfumo huo ni kama mgongo wa Taasisi maana unahusika na makusanyo ya fedha hivyo lazima kuwepo na mpango wa kunusuru hatari yoyote inayoweza kujitokeza hasa katika majanga.
Picha ya pamoja ya maafisa wanaotumia mfumo wa pamoja wa kusimamia huduma za ankara za Maji kwa Mamlaka za Maji nchini mara baada ya kufunga mafunzo.

“Katika hili suala la kuwa na Disaster Recovery Plan & Backup ipewe kipaumbele ili tuwe salama inapotokea majanga”.

Awali mratibu wa mafunzo Mhandisi Masoud Almas amemweleza Katibu Mkuu kwamba mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha Mamlaka zote nchini zinaanza kutumia mfumo huo na kuondokana na mifumo ya wakandarasi binafsi.

Amesema kwa sasa Mfumo unatumiwa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 46 kati ya 95 (sawa na asilimia 48). Lengo ni kuhakikisha mamlaka zote zinapewa mafunzo ya kutumia mfumo hatimaye Mamlaka zote nchini zitumie mfumo huo mmoja.

Amezita faida za mfumo huo kwamba taarifa zote za mteja zinaweza kupatikana kielektloniki , kupitia kompyuta au simu yake ya mkononi. Mteja Anaweza kununua maji au kufuatilia taarifa za bili yake kupitia Simu ya mkononi.

Kwa upande wa Bodi za mabonde amesema tayari Mafunzo yameshafanyika kwa Bodi za Mabonde zote 9 na wako kwenye hatua za kufanya Upimaji wa Kukubali kwa Mfumo kwa Mtumiaji (User Acceptance Testing) na Wizara ya Fedha (Timu ya GePG) ili waweze kupata Kibali cha kuanza kutumia Mfumo kabla/ifikapo Julai 2021 maana ni moja ya masharti ya Wizara ya Fedha.

Mafunzo haya ni mwendelezo wa mafunzo ambayo yamekuwa yakifanyika sehemu mbalimblai nchini yakilenga kuwafikia wataalam wote wanaoshughulika na mifumo ya malipo ya bili za maji ambapo Awamu hii jumla ya mamlaka 19 zimeshiriki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news