MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO KWA NIABA YA RAIS SAMIA APOKEA GAWIO LA SERIKALI KUTOKA BENKI YA NMB

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh21.8 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana ambalo lilikuwa shilingi 15.25 bilioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.

Akipokea mfano wa hundi, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwa mwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchi majirani.

Dkt. Mpango amesema, kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazima waongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Viongozi Wakuu wa Benki ya NMB muda mfupi baada ya kupokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.

Gawio lililotolewa ni sehemu ya faida ya Sh206 bilioni ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa kuishia desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.

Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayo kwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.
“Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya, lakini nataka muongeze ubunifu ili mwakani muwe zaidi ya hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazi nzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa,” amesema Dkt. Mpango.

Kuhusu NMB amewataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na Benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu riba kubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.

Amewataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathimini vinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kama kumejaa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Edwin Mhede amesema, tayari fedha hizo zilishawekwa katika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana na mwenendo wavyoona.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Viongozi Wakuu wa Benki ya NMB muda mfupi baada ya kupokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.

Mhede alitaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katika kuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa Serikalini shilingi 245 bilioni kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya shilingi 2 bilioni kwenye huduma za kijamii.

Bi. Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh1.1 trilioni kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015 hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwa viwango vinavyotakiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news