Makamu wa Rais Dkt.Mpango awasili nchini Ufaransa kuhudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango Juni 29, 2021 amewasili Paris nchini Ufaransa ambako atahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa kuanzia leo Juni 30 hadi Julai 2, 2021.
Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo mara baada ya kuwasili Paris Nchini Ufaransa Juni 29, 2021.

Aidha, Makamu wa Rais alipata maelezo jinsi Ubalozi wa Tnazania unavyotekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake uwakilishi ambalo ni Ufaransa, Hispania; Ureno; Algeria na Morocco. Maelezo hayo yalitolewa na Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Pia Balozi Shelukindo anaiwakilisha Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa, Mheshimiwa Shelukindo akitoa maelezo kuhusu uwakilishi wa Tanzania katika Nchi za Ufaransa , Uhispania, Tunisia na Moroco mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili Nchini Ufarasa Juni 29,2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu pamoja na ujumbe ulioongozana na Makamu wa Rais nchini Ufaransa kulia ni kinara wa uwezeshaji kiuchumi Bi. Anjela Kairuki na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N Mbarouk.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Balozi Shelukindo kwa uwakilishi mzuri katika nchi hizo na kumuhakikishia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazojitokeza katika ubalozi huo. 

Amemtaka kuendelea kutafuta mahusiano na sekta binafsi zilizopo nchini Ufaransa kwa manufaa ya nchi zote mbili. 

Leo Makamu wa Rais anatarajia kuhudhuria ufunguzi wa Jukwaa la kizazi cha usawa lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news