Msanii Nikk wa Pili ateuliwa DC Kisarawe, Jokate apelekwa Temeke

Na Mwandishi Diramakini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Msanii Nickson Simon John maarufu Nikk wa Pili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
DC mteule Nikk wa Pili anachukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Vilevile, Rais Samia amewateua baadhi ya waliokuwa wabunge lakini kwa sababu mbalimbali wakashindwa kurejea bungeni. Wateule hao ni Joshua Nassari (Bunda), Halima Bulembo (Muheza) na Peter Lijualikali (Nkasi).

Rais Samia amewateua pia waliokuwa viongozi wa upinzani wakahamia CCM. 

Wateule hao ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dkt. Vincent Mashinji (Serengeti), aliyekuwa meya wa Arusha, Kalist Lazaro (Lushoto), aliyekuwa mwanasheria wa ACT Wazalendo, Albert Msando (Morogoro).

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwigizaji Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Basilla Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Basilla aliwahi kuwa Miss Tanzania 1998.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news